Zilipendwa

Zilipendwa
By Diamond Platnumz et al.

Ooh, hizo ni zama za kale,
Ohh, sangulo na pepe kalee
Zilipendwa

Rayvanny:
Eeh kizamani, kutoa kadi na maua
Zilipendwa
Wanataka mali, ukilipa unakwarua
Zilipendwa
Ufundi kitandani, sio maguvu kujikwamua
Zilipendwa
Unafika ndani, hujatomasa unachanua
Zilipendwa
Wanawake wa leo, wanataka mikakati,
Ukiwa mzogaji, haki ya mungu huwapati,
Mapenzi ya video yatakutoa kamasi,
Eti nikinywa maji, nakuona kwenye glasi
Zilipendwa
Eeh kupiga chabo ghetto
Zilipendwa
Mkono na dettol
Zilipendwa
Sunche na kapeto
Zilipendwa
Majay na Mobeto
Zilipendwa

Diamond:
Ooh, hizo ni zama za kale
oooh, sangulo na pepe kale
Mmmhh Bolingo ndombolo
Zilipendwa
Twanga chipolopolo
Zilipendwa
Na maji ya kandoro
Zilipendwa
Simba wa Morogoro
Zilipendwa

Rich Mavoko:
Mtaani sipati sukari guru kabisa
Zilipendwa
Hivi yuko wapi, Mb Dogg wa Latiffa
Zilipendwa
Babu Tale wapi papa misifa
Zilipendwa
Siku hizi party, hatuendagi Ibiza
Zilipendwa
Mpira na Pele
Zilipendwa
Tanu Nyerere
Zilipendwa
Asha ngedere
Zilipendwa
Alusi mabele
Zilipendwa
Eeti uuze nyumba, ueke heshima bar
Eeti mlazimishe alokukataa
Sabuni kicherema
Zilipendwa
Mabanda ya sinema
Zilipendwa
Lipumba na mrema
Zilipendwa
Diamond na Wema
Zilipendwa

Diamond:
Ooh, hizo ni zama za kale
oooh, sangulo na pepe kale
Wakina Soggy doggi
Zilipendwa
Chaneli ya analogi
Zilipendwa
Movie za cyborgi
Zilipendwa
Van Damme Arnoldi
Zilipendwa

Queen Darleen:
Unanibeep nikupigie, umeiweka vocha?
Ule wewe nilipe mie, umeniona lofa?
Tena na madada wenye majina acheni visa
Unaitwa ukale dinner mnakwenda tisa
Nywele za kichina
Zilipendwa
Pochi za kuazima
Zilipendwa
Zena na betina
Zilipendwa
Bashite gwajima
Zilipendwa

Diamond:
Ooh, hizo ni zama za kale
oooh, sangulo na pepe kale
Mm Amita Bachani
Zilipendwa
TV kwa jirani
Zilipendwa
Madee Rayvanny
Zilipendwa
Zari Ivanny
Zilipendwa

Harmonize:
Ya nini kunichunguza naishi wapi
Zilipendwa
Nala chapati kwa mahindi au makapi
Zilipendwa
Kutwa kunikalia una kamati
Zilipendwa
Ooh ya Rabi masikini, kuni dhihaki
Aah Samba mapangala
Zilipendwa
P Funk Kajala
Zilipendwa
Onyango na Jangala
Zilipendwa
Rufufu Mkandala
Zilipendwa
Vya nini vidomo domo, nitupiani tunguli
Kisa pesa za mkopo msimu wa magufuli
Aah Bongoman yondo
Zilipendwa
Sikinde msondo
Zilipendwa
Magari ya udongo
Zilipendwa
Babu wa loliondo
Zilipendwa

Diamond:
Ooh, hizo ni zama za kale
oooh, sangulo na pepe kale
Aah TV za kichogo
Zilipendwa
Wakina Man Dojo
Zilipendwa
Aggy na lyobo
Zilipendwa
Akina Hatupogo
Zilipendwa

Mbosso:
Eeti msiba ukiona Bundi unataka kupagawa
Tulale makundi makundi, kuogopa popo bawa
Zuwena ntampata wapi
Zilipendwa
Zueena wa zile nyakati
Zilipendwa
Kujifanya mapanga sunna eti wamepinda
Wengine wabeba vyuma na hakuna marinda
Iddi Amini dada
Zilipendwa
Miuno ya H Baba
Zilipendwa
Domo Chai Jabba
Zilipendwa
Michezo ya kibaba baba
Zilipendwa

Lava Lava:
Wale wapiga madeal, sasa hali mbaya
Zilipendwa
Hizi zama za magufuli, si za jakaya
Zilipendwa
Ugomvi wa Mr. Nice na Dudu Baya
Zilipendwa
Vikatuni vya madenge baba ubaya
Zilipendwa
Muhogo mchungu Mr. Bean, wapi bambo
Wale wazamiaji wa melini, wazee wa ng’ambo
Hivi yuko wapi Benjamini wa Mambo Jambo
Wa Vietnam waporini vita na Rambo
Eh ndanda Mjela jela
Zilipendwa
Kidali kombolela
Zilipendwa
Max na Zembwela
Zilipendwa
Juma Nature na Fela
Zilipendwa

Diamond:
Ooh, hizo ni zama za kale
oooh, sangulo na pepe kale
Mmmh kamanda Daz Nunda
Zilipendwa
Kalumanzila ndumba
Zilipendwa
Simu za dole gumba
Zilipendwa
Johari na Kanumba
Zilipendwa